5 Februari 2019 - 16:42
Mwanasiasa aliokuwa dhidi ya Uislamu asilimu nchini Netherlands

Mmoja miongoni mwa wabunge wa zamani wa bunge la Netherlands ambaye alikuwa katika wabunge wanaopambana dhidi ya Uislamu, ghafla ameonekana kutangaza kubadili dini na kujiunga na dini tukufu ya kiislamu nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mbunge huyo wa zamani ambaye ni mwanachama wa chama cha kisiasa cha “PFF” nchini humo, hapo awali alikuwa anaamini na kusema kuwa Qur`an ni sumu ya jamii ya kibinadamu na dhidi ya uwanadamu, ama baada ya kufanya uchunguzi wake wa kina kuhusu dini ya kiislamu, ambapo lengo lake lilikuwa ni kuandika kitabu dhidi ya Uislamu, hatimaye amefahamu ukweli na uhakika wa Uislamu na hatimaye amejiunga na Uilamu, huku akisema kwamba, kwa hakika najisuta na yale niliokuwa nimeyafanya hapo mwanzo dhidi ya Uislamu.
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 40 na aliyekuwa mbunge wa chama cha PFF ameyasema hayo alipokuwa anafanya mahojiano na gazeti la NRC huku akisisitiza nilipokuwa nafanya uhakiki wa kuandika kitabu dhidi ya dini ya Kiislamu ndipo nikabaini ukweli wa Uislamu hatimaye kujiunga na dini hiyo.   
mwisho/290